Kituo cha Taarifa za Dharura Zinazotumika
Wakati wa janga au dharura, tembelea ukurasa huu ili kupata taarifa rasmi za karibuni zaidi kutoka kwa Jiji la Austin na Kaunti ya Travis kuhusu hatari inayoikabili jamii yetu na hatua za haraka unazopaswa kuchukua ili kukuhifadhi wewe na wapendwa wako salama. Zingatia kualamisha kiunganishi cha ukurasa huu ili uweze kukipata kwa haraka wakati wa janga. Unaweza pia kufuata Austin HSEM katika mitandao ya kijamii:
Twitter - @AustinHSEM
Facebook - @AustinHSEM
Jitayarishe Sasa kwa Ajili ya Dharura
Njia bora zaidi ya kujilinda mwenyewe wakati wa dharura kuu ni kuwa na mpango wa usalama, vifaa, na ufikiaji wa taarifa muhimu muda mrefu kabla haijatokea.
Tembelea ReadyCentralTexas.org ili kujiandikisha kupokea taarifa za dharura, na ujifunze unachoweza kufanya leo ili kujisaidia mwenyewe kuokoka na kupona kwa haraka zaidi kutokana na majanga katika siku zijazo.
Ofisi ya Msajili wa Msaada wa Dharura wa Jimbo la Texas
Jisajili kwa Ofisi ya Msajili wa Msaada wa Dharura wa Jimbo la Texas (STEAR). Jisajili kwa STEAR ikiwa wewe, mwanafamilia au rafiki ana hali ya kiafya, mahitaji ya kutembea, au mahitaji ya mawasiliano yanayohitaji msaada wa ziada wakati wa tukio la dharura.
Pakua Programu ya Ready Central Texas
Ofisi ya Jiji la Austin ya Usalama wa Nchi na Usimamizi wa Dharura na Ofisi ya Usimamizi wa Dharura ya Kaunti ya Travis zimeshirikiana kuanzisha programu ya simu ya matayarisho ya dharura.
Programu ya Ready Central Texas huandaa:
- Ripoti za habari na maonyo
- Habari za maandalizi
- Orodha za ukaguzi za mpango wa dharura ili kusaidia kuhakikisha kwamba una kile unachohitaji
Programu hio inapatikana kwenye vifaa vya Android na iOS na ni bure kupakua na kutumia.
Hali
Vituo vya Kupasha joto
Msimu wa baridi kali umetabiriwa. Vituo vyote vya mbuga na maktaba vinaweza kutumika kama Vituo vya Kupasha Joto wakati wa masaa ya kawaida ya kazi. Wanyama wa huduma wanaruhusiwa katika vituo vya Jiji. Angalia saa za kazi kabla ya kuwasili. Tafadhali fuatilia habari za eneo lako kwa taarifa ya hali ya hewa iliyosasishwa na utembelee ReadyCentralTexas.org kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa hali ya hewa ya majira ya baridi.
Ramani ya Vituo vya Kupata Joto
Maelezo ya Ramani
= Kituo cha Kupasha cha Bustani kilicho na saa za kazi za kawaida
= Kituo cha Kupasha cha Maktaba kilicho na saa za kazi za kawaida
= Kituo cha Kupasha cha Bustani kilicho na saa za kazi zilizoongezwa
= Kituo cha Kupasha cha Maktaba kilicho na saa za kazi zilizoongezwa
= Biashara imefungwa kwa muda au haipatikani
Vituo vya Kaunti:
Vituo vya Jamii vya Kaunti ya Travis vitatumika kama Vituo vya Kupasha wakati wa saa za kawaida za kazi. Angalia saa na shughuli kabla ya kuwasili.
Updated 8:56 p.m. 11/22/2024