Katika hali ya dharura usisite kupigia 9-1-1 simu. Tovuti hii itakusaidia kuelewa ni lini unapaswa kupigia 9-1-1 simu kwanza na unachoweza kufanya ili kuwasaidia wapokeaji simu kutuma wahudumu wa huduma ya kwanza kwako haraka iwezekanavyo. Huduma za Polisi, Zimamoto, Matibabu ya Dharura na Afya ya Akili zinapatikana kwa masaa 24 siku siku saba kwa wiki.
Dharura ni nini?
Dharura inaweza kumaanisha mambo tofauti kwa watu tofauti kulingana na hali. Hata hivyo, kuna nyakati fulani kila mtu anafaa kugeukia 9-1-1 ili kupata usaidizi. Pigia 9-1-1 simu Mara moja ikiwa hali inahusisha:
- Hatari ya moja kwa moja kwa maisha au mali
- Moto
- Uhalifu unaoendelea
- Dharura ya matibabu
- Mtu anayehitaji huduma za afya ya akili
Ikiwa huwezi kupiga simu, Tuma ujumbe mfupi kwa 9-1-1. Ujumbe wa maandishi pekee, usijumuishe picha au video. 9-1-1 kwa maandishi inapatikana kwa lugha ya Kiingereza pekee kwa wakati huu.
Cha Kusema utakapopiga simu
Moja ya mambo muhimu unayoweza kufanya ni kubaki mtulivu. Ongea kwa uwazi na utoe maelezo mengi uwezavyo kuhusu kinachoendelea na kuhusu eneo lako ikiwa ni pamoja na anwani, makutano makubwa, au alama muhimu. Kutoa maelezo haya huwasaidia wapokeaji simu kutuma wahudumu wa huduma ya kwanza kwenye eneo haraka iwezekanavyo. Kumbuka, kipaumbele cha 9-1-1 ni kukupatia usaidizi unaohitaji. Wapokeaji simu hawajali na hawatauliza KAMWE kuhusu hali yako ya uhamiaji.
Rasilimali Zisizo za Dharura
Ikiwa huna dharura ya haraka lakini bado unahitaji usaidizi kuna rasilimali kadhaa zinazopatikana:
Austin 3-1-1
Piga 3-1-1 au 512-974-2000
Unapopiga 3-1-1, simu yako inajibiwa na balozi wa Jiji la Austin. Mabalozi wanapatikana ili kujibu swali lolote, au kusaidia kwa suala lolote ambalo unaweza kuwa nalo kuhusu idara au huduma za Jiji la Austin masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki, siku 365 kwa mwaka. Unaweza pia kukamilisha Ombi la Huduma mtandaoni kwa huduma nyingi za Jiji la Austin. Unaweza pia kutumia programu ya simu ya Austin 3-1-1 kuripoti mashimo barabarani, grafiti, mbwa koko na zaidi. Tembelea tovuti ya Austin 3-1-1 ili kujifunza zaidi kuhusu huduma zake zote.
iReport Austin
Tembelea ireportaustin.com
Unaweza kuandikisha ripoti ya matukio yasiyo ya dharura kwa Idara ya Polisi ya Austin(APD) masaa 24 kwa siku, siku saba kwa wiki mwaka mzima kwa kutumia mfumo wa kuripoti matukio mtandaoni wa APD ireportaustin.com. Lango hili ni la matukio yaliyopita, wakati watuhumiwa hawapo tena kwenye eneo la tukio au kuonekana, au wakati hakuna tishio la moja kwa moja kwa maisha au mali. Mifano ya ripoti ni pamoja na:
- Shambulio au vitisho
- Vitisho (Tishio la Kigaidi na Shambulio la Vitisho)
- Kuvunja nyumba
- Uhalifu
- Ulaghai
- Unyanyasaji
- Ajali ambapo dereva anaondoka kwenye eneo la tukio (Hit & Run)
- Tukio linalohusisha gari
- Mali iliyopotea
- Wizi
Huduma za Afya ya Akili
Piaga simu 512-472-HELP (4357)
Ikiwa wewe au mtu unayemjua anakabiliwa na tatizo la afya ya akili, au anahitaji huduma za haraka za afya ya akili, usaidizi unapatikana kupitia nambari ya simu ya 512-472-HELP (4357) ya Huduma Muhimu 24/7.
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma za afya ya akili ya jamii, tembelea tovuti ya Huduma Muhimu.